Monday, January 19, 2015

HAFSA KAZINJA AFUNGUKA MAZITO..."NATESWA NA MAJINI NINAPOKUWA JUKWAANI"


Hafsa Kazinja akipozi.
MWANAMUZIKI aliyeamua kumgeukia Mungu na kuokoka, Hafsa Kazinja amefunguka kuwa alikuwa akiteswa na mauzauza ya kishirikina pindi alipokuwa katika majukwaa akiimba Bongo Fleva.
Mwanamuziki aliyeamua kumgeukia Mungu na kuokoka, Hafsa Kazinja.
Akipiga stori na paparazi wetu, Hafsa alisema alikumbana na mambo mengi sana ya ajabu ikiwemo kuona majoka makubwa jukwaani akiwa anatumbuiza na sauti za ajabu za mara kwa mara.
“Nilikuwa naishi maisha ya ajabu sana jamani yaani, nikiwa jukwaani naimba basi naanza kusikia sauti za ajabu mara naona majoka makubwa yanapita pita mbele yangu na kunifanya niishiwe pozi katika utumbuizaji wangu, hayo yote najua zilikuwa chuki za binadamu, nashukuru tangu niokoke hivi sasa sina matatizo hayo kabisa,” alisema Hafsa.