Wednesday, January 14, 2015

HAYA NDIO MAJANGA YALIYOMKUTA RAPPER FID Q.



Baada ya msanii Ambwene Yessaya aka A.Y kutangaza jana kuwa namba yake ya simu imekuwa hacked na mtu ambaye akijitambulisha kwa watu kuwa yeye ni A.Y huku akiwaomba hela, sasa taarifa nyingine ninayotaka kukusogezea ni kutoka kwa rapper Fareed Kubanda aka Fid Q ambaye naye amekumbwa na tukio hilo leo Jan 13. 

Sekunde chache zilizopita kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Fid Q aliwahabarisha mashabiki wake kuhusu namba yake ya simu ya mkononi kutumiwa na mtu mwingine asiyemfahamu;”TAARIFA: Jamaa wamehack namba yangu ya tiGo ambayo ndo ilikua na whatsapp.