Wednesday, January 21, 2015

INASIKITISHA SANA...!!!! WANANDOA [PICHANANI] WAUWAWA KIKATILI SIKU CHACHE TU BAADA YA NDOA YAO KUFUNGWA

Ndoa mpya ya wanandoa kutoka Afrika kusini kwa majina ,Wamukelwa Memela na  Wendy Campbell,waliofunga ndoa mwezi wa 12 Disemba ya mwaka jana wameuawa mwaka huu Januari 15 ya mwaka huu na wavamizi waliovamia nyumba yao.Wanandoa hao walinyongwa mpaka kufa na majambazi hayo yaliyo acha simu zao tu zikiwa wazi hebu fikiria hii jamani inahuzunisha sana endelea.....
Kwa mujibu wa baba wa mume,Sandile Memela,uchunguzi wa polisi mwanae mwenye miaka 29 alikuwa na ugomvi na mmoja wa majambazi hayo,ambaye ndiye aliyemvamia na kumpiga na kifaa cha bustani kisha kumvutia chumbani kwenye kitanda chake na kumfunga pembeni ya mke wake
Kwa mujibu wa muandishi wetu aliye Afrika kusini anadai kuwa baada ya majambazi kuharibu simu zao,kuiba vifaa vya ndani na kuvuruga nyumba yao vibaya kisha waliwa uwa kwa pamoja
Baba wa marehemu anadai kuwa walikuwa wamepanga mipango yao ya mwaka huu,ndo hivyo tena mambo yameenda kombo "ama kweli ng'ombe wa masikini hazai".Hata hivyo uchunguzi wa polisi bado unaendelea