Dunia na teknolojia yake, kila siku kuna mapya kwa hiyo hatutoacha kushangazwa nayo kila yanapojitokeza.
Nikufahamishe kwamba hii ndege inaitwa ‘Solar Impulse 2′, inatumia mwanga wa jua tu kuzalisha nguvu ya umeme ambayo inaifanya iruke.
Hii ina umbile ambalo ni sawa na ukubwa wa ndege ya Boeing 747, lakini uzito wake ni wa kawaida kama gari kubwa.
Mpango walionao ni kuirusha kutoka Abu Dhabi na itazunguka dunia nzima mtu wangu kwa kutumia nguvu hiyo hiyo inayotokana na mwanga wa jua.