Monday, January 19, 2015

SUMATRA IMEZIFUNGIA DALADALA ZINAZOFANYA SAFARI ZAKE KIMARA HADI KARIAKOO KWA SIKU 30 KUTOKANA NA KUWATOZA ABIRIA NAULI YA SH. 800

 
(Sumatra)Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imeifungia daladala inayofanya safari zake Kimara hadi Kariakoo kwa siku 30 kutokana na kuwatoza abiria nauli ya Sh. 800 tofauti na iliyopangwa na mamlaka hiyo. 
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Michael Kisaka, daladala hilo lenye namba za usajili T 276 AYT linalofanya safari zake Kimara-Kariakoo lilikamatwa kwa kosa la kutoza nauli zaidi ya kiwango kilichoridhiwa na mamlaka hiyo. 
Taarifa hiyo ilieleza kuwa abiria walitozwa nauli ya Sh. 800 badala ya Sh. 500 kwa safari ya ruti hiyo. 
“Huo ni ukiukwaji wa Kanuni namba 34 na 35 ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji kwa Magari ya Abiria ya mwaka 2007,” alieleza. 
Mamlaka inatoa adhabu ya kufungia basi hilo T 276 AYT lenye leseni namba A2A044023 kwa muda  wa siku 30 kwa njia zote za Tanzania  Bara na kwamba adhabu hii itaanza leo. 
Aidha, mmiliki alitakiwa kuwasilisha barua yenye maelezo na vielelezo kuhusu hatua zilizochukua dhidi ya dereva na kondakta wa gari lako kwa kosa hilo.