Sunday, February 1, 2015

AFRICA KUJITOA MAHAKAMA YA ICC IFIKAPO JUNE 2015 -ROBERT MUGABE (MWENYEKITI AU)

Ethiopia Mugabe AU
  
 Mwenyekiti Mpya wa Umoja Wa Afrika(African Union) amesema Africa itajiondoa International Criminal Court (ICC). 

Amesema hiyo itakua agenda katika mkutano wa umoja huo utakaofanyika mwezi wa sita mwaka huu nchini Afrika Kusini. 

Rais Mugabe(Zimbabwe), ameyasema hayo  tarehe 31 Januari, 2015 wakati wa kufunga mkutano wa 24 wa umoja huo Addis Ababa nchini Ethiopia.

Ametoa wito kwa Africa kuunda "The African Court of Justice and Human Right" itakayoshughulikia kesi za Afrika ambazo zinafanana na zile za ICC. 

Akiunga mkono hoja hiyo, Raisi wa kenya, Uhuru Kenyatta ameahidi kutoa $ 1M kwa ajili ya uanzishwaji wa "The African Court of Justice and Human Right".