Sunday, February 1, 2015

SERIKALI INATARAJIA KUWASILISHA MSWAADA KULIOMBA BUNGE KUKUSANYA SH 100 KATIKA KILA LITA YA MAFUTA ILI KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI



Serikali kupitia wizara ya fedha inatarajia kuwasilisha mswaada Bungeni kabla ya alhamisi ya february 5 mwaka huu, kuliomba bunge liirusuhusu serikali kukusanya shilingi mia moja katika kila lita ya mafuta kutokana na punguzo kubwa la mafuta katika soko kwa nia ya kupata shilingi bilioni 120 zitakazowezesha kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Tanzania kupitia mradi wa wakala wa nishati vijijini (REA).
Kutokana na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi wa nishati ya umeme vijijini unaotarajiwa kumalizika kabla ya june mwaka huu kwa kusambaza umeme katika vijiji vyote Tanzania serikali itawasilisha mswaada wa kuliomba bunge kuidhinisha ongezeko la shilingi mia moja ili kupata shilingi mia moja na hamsini kwa kila lita kusaidia kuukamilisha mradi huo wa nishati ya umeme vijiji.
Awali katika kikao cha ndani baadhi ya watendaji wa wakala wa nishati ya umeme vijijini pamoja na shirika la umeme nchini Tanesco wamejikuta katika hali ngumu kutoka kwa naibu waziri huyo baada ya mbunge wa Gairo Mh Ahmed Shabiby kulalamikia watendaji hao kwa kuzembea na kutokuwa na nia thabiti ya kuukamilisha mradi huo kwa wakati licha ya agizo la rais jambo linalokwamisha maendeleo kwa wananchi kwa kukosa nishati ya umeme huku baaadhi ya vijiji vikirukwa bila ya sababu.
Nao baadhi ya wananchi wameonesha kutokuwa na imani na baadhi ya wataalam na watendaji wa wakala wa nishati ya umeme vijijini pamoja na Tanesco kutokana na ahadi nyingi hewa wanazopewa na kuishia kusimikwa kwa nguzo za umeme ama kuwekwa alama bila ya kuunganishiwa nishati hiyo.