Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Aunt ezekiel
amejikuta akitoa maneno makali baada ya mashabiki wake kumshabulia kwa
maneno baada ya kuweka mtandaoni picha ikimuonyesha amevalia kinguo
ambacho kwa maoni ya mashabiki hao hakistahili kuvaliwa na mwanamke
mjamzito na kibaya zaidi alionekana mkononi ameshika shupa ambao wengi
waliiona kama niyakilevi.
Aunty Ezekiel alibandika picha hiyo hapo juu hivi juzi kati akiwa na
jamaa kwenye ukurasa wake mtandaoni na kuandika maneno “My best
friend,my love,my kimoko I love him so much”
Baada ya kubandika ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake walionyeshwa
kukera na mavazi na sehemu alikokuwepo nalumtaka atulie nyumbani alee
mimba yake kwani kwasasa inaonekana kuwa na ya zaidi ya miezi nane na
wiki kadhaa.
“Ungetulia tu nyumbani ukasubirikujifungua salamamjamzito kuzurura
namna hiyo na mijanaume sio poakabisa tena na kilaji mkononi harafu pia
hata hayo mavazi mmmh!!” alisema mmoja wa shabiki na kuungwa mkono na
wengine wengi.
Baada ya muda kidogo aunty ezekel akaibuka na kuandika ; “Plz msiwe
bac mnaongea kitu kabla ujajua undani wake, ni vizuri kuuliza kuliko
kuandika tu ilimradi na wewe uonekane umeongea hiyo nguo ni special kwa
mama mjamzito na hapo juu inampira wakutosha tu na mapajani ndio inabana
sasa”
Lakini majibu hayo yalionekana kuamsha maneno zaidi ya kumponda Aunty
ambae nae mwishoni alionekana kushindwa kuvumilia na kutoa maneno
machafu ambayo sio busara kuyabandika hapa.
Wewe je umeionaje picha hiyo ya Aunty?
