Friday, February 13, 2015

KAJALA AFUNGUKA NA KUDAI ANAHITAJI MDOGO WA PAULA

Mwanadada anayeendesha maisha yake kwa
kuuza sura kwenye filamu za Kibongo, Kajala
Masanja amefunguka kuwa ni muda muafaka
wa kufanya mishemishe za kumtafuta mtoto
mwingine kwani yule wa kwanza , Paula
ameshakua.
Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.
Akizungumzia mipango yake kwa sasa hasa
kwenye suala la kuongeza mtoto, Kajala
alisema umri unazidi kuyoyoma na Paula
anazidi kuwa mkubwa hivyo ni vyema
akamtafutia mdogo wake fasta kabla ya
kuamua kutulia .
“ Kwa kweli nahitaji kumpata mdogo wake
Paula haraka , umri unazidi kusonga mbele ,
siyo nakuja kuzaa tena Paula kishakuwa
mdada mkubwa , itakuwa aibu , ” alisema Kajala .