Mwanadada anayepiga dili la utangazaji kupitia Zouk TV ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa mimba ya shosti wake, Wema Sepetu inampa ‘uchizi’ kwa kutamani kila kukicha na yeye anase ujauzito.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Penny alisema kuwa hivi sasa karibia rafiki zake wote wana watoto kitu kinachomchanganya na kumtamanisha na yeye atundikwe kibendi.
“Unajua Wema atakapojifungua na kuna rafiki zangu wengine wana watoto nikikaa nao stori nyingi zitakuwa ni za watoto zao, mimi nitaongea nini sasa? Ndio maana nilipopata taarifa za ujauzito wake nilifurahi sana, pia amenipa mshawasha,” alisema Penny.