Ligi Kuu Ubelgiji imeendelea tena leo February 6 kwa michezo kadhaa kupigwa, miongoni mwa michezo iliyochezwa leo February 6 ni mchezo kati ya Mouscron FC dhidi ya klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta,
Mtandao wa Millard Ayo ulielezakuwa mchezo huu ulikuwa na mvuto kwa Tanzania zaidi kwani ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta kucheza toka amejiunga na klabu hiyo.
Mbwana Samatta ambaye ndio nahodha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania, alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu yake mpya ya KRC Genk akitokea benchi, Samatta aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis ambaye alitoa pasi ya goli la ushindi kwa KRC Genk dakika ya 63 na Thomas Buffel kupachika mpira nyavuni.