Saturday, February 7, 2015

WACHEZAJI WA SIMBA WAKIWA KATIKA MAZOEZI JIJINI TANGA

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic (mwenye mpira) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mchezo wa leo dhidi ya Coastal union.
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Emannuel Okwi (katikati) akijaribu kumtoka kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude na beki, Hassani Kessy kwenye Uwanja wa Popatlal, Tanga.
Kocha wa Simba, Goran Kopunovic akifanya mazoezi pamoja na beki wa kushoto wa timu hiyo, Issa Rashidi 'Baba Ubaya' yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Popatlal, Tanga kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Coastal utakaopigwa leo.
Kocha, Goran Kopunovic akimuelekeza jambo kiungo wa timu hiyo, Mganda, Simon Sserunkuma baada ya mazoezi ya timu hiyo jijini Tanga.