Thursday, February 19, 2015

WANA KAMA TATIZO NYOTA BONYEZENI RELI!

OYOOOO aje mabraza na masista? Kama kawa, kama dawa tunamiti wansi ageini katika kijiwe chetu na kubonga mastori ya tauni ama nini? Niaje masela wangu wa kipande cha TA mapenzi yalikozaliwa? Mko poa?

Veri sori kwa maraia mliofesi mbishe za mabomu ya hapa na pale kozi najua ni jinsi gani pipo ambao hawana expiriensi na michongo ka hiyo wanavyokuwa na kiraruraru pindi kinaponukishwa.
Lakini kimsingi inabidi kidogo tuwekane kwenye reli kiaina. Michongo kama hii si ya kuichukulia poa, inakata stimu kinomanoma.

Kila raia anajua kwamba kuna michongo kibao ambayo haiendi sawa lakini samtaim inabidi tuwe na rispekti katika kila hatua ambayo tunataka kuisongesha.Tunapokuwa tumewaka na stimu zetu, ile kitu roho inapenda, tusizipige teke busara zetu kozi mwisho wa siku wote tunaishi chini ya mwavuli wa Bongo na tutadanja hapahapa Bongo.
Najua masela kibao mmekata ringi, hakuchi kunakucha siyo kesi bati tuseme na arosto zetu maana ringi lipo tu lakini utu unapaswa kusimama kwenye laini. Matukio ya mfululizo ya wana kuwadandia mamwera na kuwakwapulia vya moto kisha kuwakili baadhi yao inaleta picha mbaya kitaa. Mbaya zaidi wana wanaofanya michongo hii tunawajua lakini tunawafumbia macho kozi wanatupoza vihela mbuzi.
Niwaambie tu wana, kama kusoma hatujui, hata hatuoni picha? Kuna mifano kibwena tu ambayo imeshahapeni na kuonesha kwamba Wabongo wengi hawana expiriensi ya kufesi matukio ya kivita.
Kitu cha panya rodi tu kilichohapeni juzikati Bongo ilikuwa ni mperampera. Kimetoa picha jinsi gani hii michongo tumekuwa tukiisikia tu na kuitazama katika televisheni katika nchi za wenzetu.

Michongo ya kusikia mabomu, bomba za moto ni adimu Kibongobongo. Kikinuka kiaina tu, utashuhudia maraia wanavyotoka nduki kunusuru roho zao. Wale wenzangu na mimi fulu kuvaibreti kama simu za huu...haaa. Noma sana mazee!
Wanatamani ardhi ipasuke wajimuvuzishe insaidi. Sasa, kama ndo hivyo kwa nini tusiiweke pendingi michongo ka hiyo wakati tunajua kabisa hatuiwezi? Kwa nini tusiichunie? Kaushieni bana laifu lisonge kama kawiso.
Kwa wale mnaojitosa kulianzisha ili kutafuta gudi taimu, mbona bata lipo tu kama ukiamua kucheza karata zako vizuri. Bongo inatakiwa kuchemka.Tatizo la Wabongo wengi, krietivu imepungua. Deile watu wanaishi kimazoea, hawataki kuthubutu na kucheza madili mapya yanayoweza kuingiza ankara.
Badala yake wana mnaanza kutupa lawama kwa gavamenti kwamba haiwajali maraia wake. Kabla ya kutoa lawama faiti kwanza, piga dili monire hadi naiti kali ikiwezekana.Upoteze muda kwa kuendekeza kumbonji, saka chapaa. Meki mane mchana hadi naiti ikibidi. Kama ni kumbonji utambonji uzeeni. Komaa ili makidi wako waje wale gudi taimu, usikubali wanao waje kukopi na kupesti laifu taiti ulilopitia wewe.
Wakati nakaribia kuweka nukta, niwasihi wana waliowataiti mamwera kule TA kujisalimisha au kusalimisha silaha kwa kuzitelekeza sehemu.Tuachane na hii michongo ya kukinukisha, tujenge taratibu nzuri za kufikisha hisia zetu kwa gavamenti, watatuelewa tu.Kama vipi  nimemaliza, tugongane tena kipande hii neksti wiki, pamoko sana!