Akizungumza na Uwazi, Coletha alisema aliitwa lokesheni kucheza filamu ya Mkono wa Kushoto ambapo alikuwa tayari ameshapewa pesa ya utangulizi shilingi milioni moja na nusu.
“Niliziweka pesa kwenye begi langu la nguo. Tulifika eneo ambalo gari yetu haikuweza kupita kutokana na kuwekwa magogo njiani. Kwakuwa tulihakikishiwa usalama ikabidi tuache gari na vitu vyetu kwa muda na kusogea eneo la mbele kidogo. Kitendo cha kumaliza na kurudi tukakuta milango ya gari ipo wazi na vitu vyetu vyote havipo,” alisema Coletha.