Monday, March 30, 2015

HUKU NI TOFAUTI RAFIKI ACHA KUISHI MAISHA YA MAZOEA

HUKU NI TOFAUTI Huu ni usemi ambao nimeukuta huku kwenye dunia nyingine kabisa ya kutafuta mafanikio, unajua unapokuwa kwenye ulimwengu wa kutafuta mafanikio ni tofauti kabisa na ukiwa kwenye ulimwengu wa kutafuta ajira, kiukweli huku ni tofauti hata mimi nimeona. Unapokuwa unasoma shule wazazi na walimu wanakwambia soma sana upate kazi nzuri, upate mshahara mzuri, HUKU NI TOFAUTI, huku kwenye mafanikio unaambiwa soma sana uanzishe biashara zako, kampuni zako uwaajiri wengine. Unapokuwa shuleni unaambiwa fanya mtihani ufaulu maswali yote na hutakiwi kukosea, maana ukikosea wewe unakuwa huna akili.AISEE HUKU NI TOFAUTI.Tunapokuwa tunatafuta mafanikio tunajifunza kuwa kukosea mara nyingi ni kujifunza kufikia mafanikio yako, na matajiri wengi sana na watu wenye mafanikio wamekosea mara nyingi sana ndio wakapatia, usiogope kukosea maana ndio unaelekea mafanikio yako, wasomi wanashindwa kufanikiwa kwasababu wamebeba mentality ya shuleni na vyuoni, hivyo wanaogopa kukosea, hii inawafanya kushindwa kutumia fursa za mafanikio zinazowazunguka. Unapokuwa shuleni kumuangalizia mwenzio ni kosa la jinai bola uendeshe gari bila leseni, RAFIKI HUKU NI TOFAUTI.Kwenye kutafuta maisha lazima uwe na mtu ambae ameshafanikiwa kwenye kitu unachotaka kufanya na wewe unafanya kama alivyofanya, anakuwa mentor wako kufikia mafanikio yako na ikiwezekana na wewe unafanya zaidi yake ili uende umbali za wa ziada. Unapokuwa shuleni yule anaekosea sana ndio anaitwa mbulula, tena tunamzomea, maana hana akili, RAFIKI HUKU NI TOFAUTI, wale wenye akili kidogo shuleni tena wengine hawakusoma sana,ndio wanamiliki uchumi mkubwa maana wananidhamu na pesa. Unapokuwa shuleni ukiwa na akili saana unakuwa mmbabe kwa wenzako, hutaki tena kujifunza kutoka kwa wenzako.RAFIKI HUKU NI TOFAUTI.Hata uwe na akili vipi hata uwe na uwezo wa kufanya biashara kiasi gani, hata uwe na elimu kiasi gani, lazima ujifunze kutoka kwa wengine, kwenye kusaka mafanikio unajifunza hadi unakufa.na usipotaka kujifunza mengi yatakupita.