Tuesday, April 28, 2015

KUPA ANASWA NA MWANAUME SHOGA

Msanii wa filamu mwenye vituko kibao, Idrisa Makupa ‘Kupa’ akiwa na mwanaume tata huyo.

Msanii wa filamu mwenye vituko kibao, Idrisa Makupa ‘Kupa’  juzikati aliwaacha watu midomo wazi baada ya kunaswa akiwa beneti na mwanaume tata maarufu mjini anayefahamika kwa jina la Danny.

Wawili hao walibambwa na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar kulikokuwa na onesho la mwanamuziki Christian Bella.

Gumzo lilianza pale Danny alipomsogelea Kupa na kumnong’oneza, jambo lililowafanya watu wahoji ukaribu wa kijana huyo na msanii huyo unakujaje!

Hata hivyo, wawili hao baada ya kuona wanapigwa sana picha ‘walimtoka’ paparazi wetu hadi walipokuja kunaswa tena baadaye wakiwa wamegandana, hali iliyotafsiriwa tofauti.