Tuesday, April 28, 2015

TASWIRA YA ZARI NA DIAMOND WALIVYOJIACHIA VISIWANI ZANZIBAR, YANI NI NOMAAA.. SROTI YOTE IPO HAPA

Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond' akijiachia na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' Visiwani Zanzibar.

Diamond akilibusu tumbo la mpenzi wake Zari ambaye ni mjamzito.



Zari na Diamond wakizidi kula maisha huko Zanzibar walipokwenda kwa ajili ya shoo iliyofanyika Juni 25, mwaka huu.

STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond' na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' wamezidi kuonyesha kuwa penzi lao linazidi kuimarika baada ya Zari kuachia picha Instagram wakiwa 'close' walipokwenda Visiwani Zanzibar juzi.

Wapenzi hao walikuwa Zanzibar kwa ajili ya shoo ya Diamond iliyofanyika Jumamosi (Aprili 25, mwaka huu) usiku huko Ngome Kongwe.

Mojawapo ya picha za wapendanao hao imbayo imeenea mitandaoni ni ile ambayo Diamond analibusu tumbo la Zari mwenye ujauzito unaodaiwa kuwa wa staa huyo.