Kwenye vituo vingi vya daladala utakuta mida ya jioni wako jamaa wanachoma zao mishkaki.. na watu wamezoea kabisa unakuta watu wengi wamejipanga wanajisevia.. kua story ilitokea Temeke kwamba kuna jamaa alikuwa anatuhumiwa kwamba anauza mishkaki ya paka, ikamharibia biashara yake japo baadae iligundulika kwamba mishkaki haikuwa ya paka.
Philip Paul kagonga vichwa vya habari kwenye story za Nigeria, amesema yeye na familia yake ni walaji wazuri wa mishikaki ya chura na pia ni biashara yake inayomuweka mjini.. YES.. anauza mishkaki hiyo !!
Philip amesema shughuli ya kukamata vyura hao huwa anafanya usiku, anachotumia ni mikono tu.. wala haimpi shida sana kuwakamata.
Hii ni biashara yake kubwa, unaambiwa kaianza toka mwaka 2008, sehemu ambayo huwa anawakamata sana vyura hao ni Jimbo la Adamawa, Nigeria alafu anawasafirisha mpaka Benue, huko nd’o ambako kuna soko kubwa la mishkaki hiyo.