MMOJA wa vijana wanne walionaswa jana katika tukio la ujambazi eneo la Mataa ya Red Cross katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni anadaiwa kumvisha pete msichana mmoja ambaye ni mchumba wake.
Vijana hao walitiwa nguvuni na Jeshi la Polisi jana baada ya kuvamia na kumpora fedha raia mmoja wa kigeni eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kufanya tukio hilo, vijana hao walifanikiwa kukimbia na gari walilokuwa nalo ila kulikuwa na msamaria mwema mmoja aliyeona tukio hilo ambaye aliweza kufukuzana nao akiwa na gari yake na kufanikiwa kuwapita mbele na kuwazuia na hivyo kushindwa kupita na gari walilokuwa nalo ndipo askari kufika na kuwaweka chini ya ulinzi.
Vijana hao wanne ambao ni watanashati na ni vigumu kudhani kuwa wanaweza kujihusisha na vitendo vya ujambazi, baada ya kukamatwa na polisi walikutwa na bunduki mbili.