Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika kuuawa jana mchana na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.
Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi.
Mashuhuda wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.
Baada ya kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe