Saturday, May 23, 2015

BABA AMUUMBUA MAMA KANUMBA!

Gabriel Ng’osha na Gladness Mallya  
BABA wa marehemu mwigizaji Steven Kanumba, Charles Kanumba, amemuumbua mwanamke aliyezaa naye staa huyo, Flora Mtegoha kwa kitendo chake cha kufuatilia maisha ya msichana aliyewahi kuwa mpenzi wa mtoto wao, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Baba wa marehemu mwigizaji Steven Kanumba, Charles Kanumba.
Akizungumza kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, mzee huyo anayeishi Shinyanga, aliliambia gazeti hili kuwa ni jambo la kutia aibu kuona mzazi mwenzake akimlaumu Lulu wakati ukweli ni kuwa hakuwahi kuwa mke wala kuzaa na marehemu mtoto wao.
“Mzazi mwenzangu amekosea, Lulu hakuwa ameolewa wala kuzaa na Kanumba, siyo ukoo wake wala wa Mtegoha, kwa nini anamlalamikia? Amuache awe huru na maisha yake.“Lulu kama binti anatakiwa kuwa huru kwa kutayarisha maisha yake, mimi namuunga mkono Lulu na kumbariki katika maisha yake,” alisema mzee Kanumba.
Flora Mtegoha.
Wiki kadhaa zilizopita, Mama Kanumba aliripotiwa kufanya misa ya kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, lakini akatoa maneno makali kutokana na msichana huyo kushindwa kuhudhuria katika shughuli hiyo.
Ilidaiwa kuwa mama huyo alisema Lulu ameacha kuwa karibu naye tofauti na zamani ambako alikuwa akimjali na kumthamini, kitendo ambacho kilienda sambamba na kutoelewana kati yake na mama mzazi wa msichana huyo muigizaji.