Baada ya kukata tiketi ya kucheza fainali ya UEFA Champions League mapema wiki hii, leo hii klabu ya FC Barcelona imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Hispania.
Barcelona wametazwa rasmi kuwa Mabingwa wa La Liga baada ya kuwafunga waliokuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Atletico Madrid katika mchezo uliomalizika hivi punde.
Lionel Messi alifunga goli pekee lilowahakikishia Barca ubingwa huo katika dimba la Vicente Calderon.
Ubingwa huu unakuwa wa 23 katika historia ya klabu hiyo ya Catalunya.
Barca watakabidhiwa kombe lao watakapocheza mchezo wa mwisho wa ligi wiki ijayo.