Mh. Deo Filikunjombe ni mbunge wa wilaya ya Ludewa iliyopo kusini magharibi mwa Tanzania ambae kwa sasa ni mhula wake wakwanza katika kulitumikia jimbo la wilaya ya Ludewa akiwa kama Mbunge, mheshimiwa huyu ni mmoja wa wabunge wenye umri mdogo katika bunge la jamhuri ya wa Tanzania lakini utendaji wake wa kazi akiwa bungeni katika shughuli ya kuwawakilisha wananchi wake anafanya vizuri sana hususani katika ujengaji wa hoja zake na kuuliza maswali yenye mantiki na maslahi kwa wananchi, pia ni Mbunge mwenye misimamo yakipekee ukilinganisha na wabunge wengine wa chama chake na mwenyekujiamini kwani anajua anachokifanya kwa sifa hizi zinapelekea kuwa kipenzi cha watanzania wote hata wanachama wa vyama pinzani wanampenda sana huyu mheshimiwa kwasababu anajituma sana katika kazi, wananchi wa majimbo mengine wanadiliki kutamka wazi kwamba wanatamani hata angekuwa Mbunge wa majimbo yao, ukiangalia katika picha hapo juu utathibitisha haya, anathubutu hata kujitwisha ndoo ya maji kichwani katika shughuli za ujenzi jimboni kwake shughuli ambazo zimezoeleka kwamba huwa wanafanya wanawake lakini yeye bila kujali heshima yake ya ubunge ameifanya hii inaonyesha anania yadhati ya kuleta maendeleo na mabadiliko jomboni kwake, hongera kaka DEO FILIKUNJOMBE Pop In Town inakuombea maisha marefu na uzidi kufanikiwa katika ndoto zako siyo za kuiongoza Ludewa tu bali hata Tanzania ukiwa kama Raisi, Tanzania inakuhitaji kaka MUNGU mbariki DEO FILIKUNJOMBE, MUNGU ibariki wilaya ya Ludewa, MUNGU ibariki Tanzania.