Shilole na Snura ni watu ambao wanafananishwa na kupambanishwa na wakati mwingine kulinganishwa kwenye muziki wanaoufanya.. millardayo.com imepata nafasi ya kuongea na Snura kuhusu hili lililomtokea Shilole.
Snura ameanza hivi>>’Kiukweli kabla sijataka kusema itakuaje, mimi binafsi kutoka kwenye moyo wangu namuombea sana msamaha na Watanzania wasimuangalie hivyo ambavyo wanamuangalia‘
Sentensi nyingine Snura amesema>>’Ile ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu mzima na ana maumivu yake ndani ya moyo kwa hiyo unapozidi kumkandamiza ni kama unazidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona je itatokea tena?‘
Exclusive ya Snura na millardayo.com unaweza kuiplay hapa uisikie yote..