Saturday, May 23, 2015

Unajua Wema Sepetu Kazaliwa lini? Na Johari Je?......Unataka kujua Wanatoza Shilingi Ngapi Kucheza Muvi Moja?? Bofya hapa


Kila mwanamichezo au mwanamuziki hulipwa mshahara kulingana na kiwango chake, hali hii ipo hivyo pia kwa waigizaji na watu wengine wa kawaida.
 
Hali hii imekuwa ikiwapa morali zaidi wale wanaofanya kazi kujituma ili wapate mshahara mkubwa zaidi au kupewa kazi ya ziada tofauti na pale ulipozoea.

Hii pia imekuwa ikifanyika kwa wasanii wa filamu za Tanzania wenye umoja wao maarufu kama Bongo Movies. Hao wamekuwa wakilipwa madau kama wachezaji ili wafanye kazi za wenzao, hii imekuwa ikileta changamoto kubwa kwa wasanii kuhakikisha wanapanda dau kutokana na uwezo binafsi.
 
Asilimia kubwa ya mashabiki wa filamu za kibongo wamekuwa wakitoa fedha za kununua kazi zao bila kufahamu muhusika ‘anayemnunua’ amelipwa kiasi gani cha fedha kucheza ‘movie’ aliyoinunua. Tazama bei zao hapa chini:

Vincet Kigosi ‘Ray’
Inadaiwa kuwa huyu jamaa ni mgumu sana kukubali kucheza filamu za watu. Alishawahi kupewa Sh Milioni 10 ili cheze filamu moja (jina kapuni) lakini aligoma na amekuwa na msimamo mkubwa katika kazi zake lakini badala yake hizo fedha zikawalipa wasanii wengine watatu.
 
Inaaminika ndiye msanii mwenye gharama kubwa licha ya kuwa mpaka sasa bado amekuwa akigoma kucheza filamu za wenzake, ishu kubwa akidaiwa kujiona ni ‘staa’ zaidi ya wenzake.

Wema Sepetu
Kipaji chake kiliibuliwa na marehemu Steven Kanumba kupitia Filamu ya ‘A Point Of No Return’ baada ya hapo akapata mashavu kibao na hadi sasa amefanikiwa kucheza filamu na msanii mkubwa Van Vicker raia wa Ghana. 
 
Wema  Sepetu
Za mjini zinasema kabla hajaachana na aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Clement alikuwa akitoza kuanzia Sh Milioni Tano kwa filamu moja lakini sasa anapokea hata chini ya hapo kwa kuwa fedha zimeanza ‘kumkatikia’. 
 
Wema ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006, alizaliwa mwaka 1988, Dar anamiliki kampuni yake inayofahamika kama Endless Fame Films na ndiye mkurugenzi mtendaji.

Kajala Masanja
Ana kampuni yake ya uzalishaji wa filamu inayoitwa Kay Entertainment na tayari ameshafanya kazi zake zinayofahamika kwa majina ya Mbwa Mwitu pamoja na Pishu.
 
Lakini linapokuja suala la kufanya kazi za watu inakulazimu kuzama katika pochi au ‘waleti’ ukitoa mkono uwe na Sh Milioni Mbili lakini kwa kiasi hiki awe anakufahamu na kama ‘ndo’ mnaona kwa mara ya kwanza jiandae kuachia Sh Milioni Tatu hadi 2.5 zaidi ya hapo hakuna maneno maneno kazi inapigwa kwa kiwango kikubwa tu na binti huyu aliyezaliwa mwaka 1983.

Jacqueline Walper ‘Wolper’
Ninja, dada mkubwa, anaweza kucheza ‘sini’ zote ziwe za kijambazi, mke mwema na hata changudoa, amekuwa na mashabiki wengi sana Bongo na hata nje ambao wamekuwa wakipenda kazi zake. 
 
Mshkaji huyu ambaye alizaliwa mwaka 1987 huko Moshi, Kilimanjaro, yupo kishkaji tu kwani anakubali kupokea kuanzia Sh Milioni 2 hadi 2.5 hapo haipungui labda iongezeke ndipo atakufanyia kazi zako. Mpaka sasa amecheza filamu zaidi ya 20.

Mzee Majuto
Licha ya kuzaliwa mwaka 1948 huko Tanga, Amri Athuman ‘King Majuto’ au Mzee Majuto bado inaaminika kuwa ndiye msanii mwenye mashabiki wengi zaidi Bongo kutokana na uimara wa kuigiza hususan kwenye filamu za kuchekesha.
 
Mzee wa watu hana makuu ukitaka achekeshe weee filamu nzima jiandae kumkatia Sh Milioni 1.5 hadi 2 tu, hicho ndicho kiwango chake na atakufanyia kazi kwa umakini mkubwa zaidi ya hapo hashuki. Nje ya fani anamiliki daladala mbalimbali huko kwao Tanga ambazo pia zinamuongezea kipato.

Riyama Ally
Anaigiza kwa hisia kali sana katika kila filamu, ukitaka alie na machozi yatoke kwa wingi au acheze filamu za kimbea, majungu, vigodoro na nyinginezo wala hana makuu dada wa watu anapokea hata Sh Milioni 1.5.
 
Riyama ambaye alianza kujihusisha na maigizo mwaka 2000 akiwa na kundi la Taswira, mara nyingi katika filamu alizocheza anasifika kwa kuigiza kwa uhalisia mkubwa pengine ukimtoa Johari wa enzi za Tamthilia ya Johari basi huyu ni namba mbili kwa wepesi wa kutoa machozi. Mpaka sasa amecheza  filamu zaidi ya 40.

Blandina Chagula ‘Johari’
Alipata jina kupitia Tamthilia ya Johari kabla ya kuhamia kwenye filamu. Ni Mkurugenzi wa Kampuni ya RJ akisaidiana na msanii mwenzake Ray, katika kuindesha. Diva huyu wa movie za Kibongo alizaliwa mwaka 1983 huko Shinyanga.
 
Hana makuu katika kusaidia wenzake na mara nyingi amekuwa akijitoa kwa moyo kucheza filamu yoyote. Dau lake ni la ki-upendo zaidi kwani anapokea hata Sh Milioni Moja, hii yote anafanya kwa lengo la kusaidia wenzake. 
 
Anasifika zaidi kwa kucheza filamu za kulialia kwani kwake kutoa machozi si lolote hata sekunde mbili hazipiti anakuwa kayatiririsha hatari.