Wachezaji na viongozi wa Yanga SC wakifurahia Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga SC walikabidhiwa Kombe hilo baada ya mechi na waliokuwa wanashikilia taji hilo, Azam FC ambayo walifungwa 2-1 na washindi hao wa pili wa msimu huu. |