Tuesday, June 16, 2015

ANGALIA SOKWE ASHEREKEA MIAKA 40 TANGU KUZALIWA

Stori kutoka Uingereza nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, na kama ilivyo kawaida yangu, nafanya kushare na wewe kama hivi. 
Na stori hii inamhusu sokwe mmoja ambaye amepewa jina la Zaire, ambaye anafugwa katika bustani moja ya wanyama London, Uingereza amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 40. 

Na kama haitoshi, party yake ilikuwa poa kama ambazo huwa tumezoea kufanya binadamu, ametengenezewa keki ya nguvu katika sherehe hiyo na moja ya mabingwa wa kutengeneza keki za sherehe, Richard Burr. 

Unaambiwa sokwe huyu anapendelea vitu kama jelly zisizo na sukari, apples, na karoti hivyo mwandaaji wa keki alijikuta na jukumu la kuhakikisha anamuandalia keki itakayomfurahisha Zaire. 
Hizi ni picha za Sokwe huyo akijiachia na keki akisherehekea.