Monday, June 8, 2015

Dina Marious Afunguka Bifu Lake na Zamaradi Mketema

Aliyekuwa mtangazaji wa clouds fm, Dina Marios, leo kupitia ukurasa wake wa instagram, amefunguka kuhusu tetesi zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu bifu lake na mtangazaji mwenzie, Zamaradi Mketema pamoja na kufukuzwa kazi kwenye kituo hicho.

" Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengi yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi. Mimi sina ugomvi na Zamaradi sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.

Thats not true wala nguvu hiyo hana. Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna ugomvi.