Sunday, June 14, 2015

INASHANGAZA SANA,SOMA HAPA KUJUA SAKATA LA SITTI MTEMVU KUTAKA KUJIUWA HADI KUFA

nOT tOO lATE

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu aliyeamua kulitema taji hilo baada ya kubebeshwa kashfa amesema kuna wakati alitaka kujiua lakini alirudisha moyo nyuma na kuona ingekuwa shida kubwa nyumbani kwao.

“Sikuwa na amani, niliishi maisha ya hofu, kujifungia ndani, kulia wakati wote. Ilifikia hatua baba yangu alipata mshktuko kiasi cha kwenda kutibiwa Afrika Kusini. Mama yangu pia alipata mshtuko…ningeweza kumpoteza.”—Sitti Mtemvu.
“Mama yangu alisali na mimi, alinipigania, hakuonyesha hadharani jinsi gani anaumia, lakini ukweli ni kwamba nilimwona alivyokuwa anadhoofu na kukosa raha. Nyumba yetu iligeuka sehemu ya huzuni, amani ilitoweka ni kama tulikuwa na msiba.”—Sitti Mtemvu.
Sitti anasema siku moja mama yake alimwambia kwamba aliumia siku alipompoteza mama yake lakini machungu aliyoyasikia kwa Sitti ni mazito zaidi japo baba yake wakati wote alivumilia na hakuonesha maumivu yake.
Anasema kuna wakati baba yake alikwenda Afrika Kusini na akiwa huko alimtumia ujumbe wa kumuomba msamaha na alimwambia kwamba hizo ni changamoto.

Sitti anasema alikuwa katika wakati mgumu kiasi cha kufikia uamuzi wa kutupa laini yake ya simu ya zamani.