Monday, June 29, 2015

INASIKITISHA SANA HII.. WALIMU WABAKWA KWA ZAMU USIKU.. KISHIRIKINA

WALIMU katika shule ya msingi Nambaza
Kata ya Nansimo wilayani Bunda,
wamesema watahama shule hiyo endapo
serikali ya wilaya hiyo haitachukua hatua
madhubuti kukomesha ushirikina shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sospiter
Mafuru, alisema walimu wake wanafanyiwa
vitendo vya ushirikina ikiwa ni pamoja na
kusumbuliwa usiku na kunyolewa nywele
sehemu za siri.
Alitaja vitendo vingine kuwa ni kuvuruga
vyombo vya ndani wakati wa usiku, kumwaga
michuzi na damu kwenye mashuka na nguo za
walimu hao.
“ Vitendo hivi vimetishia usalama wa walimu hadi
sasa walimu watatu wa kike wamehama shule hii
kwa hiyo tunaomba jamii ya Nambaza wachukue
hatua,” alisema.
Alisema awali ushirikiana huo ulianza kwa
wanafunzi kuugua na kuanguka ovyo na
baadaye kwa walimu na aliomba Serikali
kuchukua hatua na kukaa na wananchi wao.
Mafuru alisema hadi sasa ana walimu
tisa,wa kike watano na wa kiume wanne.
Mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe,
alisema tayari ameviagiza vyombo vya dola
kwenda kijijini hapo kufanya utafiti kuwabaini
watuhumiwa hao.