Thursday, June 11, 2015

Irene Uwoya Apangua Tuhuma za Kuwa Amefulia Mbaya...Asema Haya

Staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya, amedai hajafulia kama baadhi ya mastaa wenzake wanavyodai.
Aliliambia gazeti hili kwamba hivi punde atathibitisha kauli yake hiyo kwa vitendo kwa kuwa alikuwa kimya kwa kuwa alikuwa anajiandaa kurudi upya kwa ladha tofauti na zilizozoeleka katika filamu.


  • “Watasema watanyamaza, ukweli ni kwamba sijafulia, kukaa kimya nina mambo yangu binafsi nafanya, hivyo nikimaliza nitarudi kwenye uigizaji,” alisema Uwoya.