Thursday, June 11, 2015

Kumbe Gari la WEMA SEPETU Kimeo..Ni Lile Alilozawadiwa Kwenye Siku ya Kuzaliwa..Sasa ni Spana Mkononi

NInoma! Kumbe lile gari la kifahari aina ya
BMW ambalo muigizaji nyota wa filamu Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ alizawadiwa wakati wa
bethidei yake na kuwa miongoni mwa sababu
za kumwagana na mpenzi wake wa awali,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ mwaka jana,
linadaiwa kuwa kimeo kwa vile limekuwa
likiharibika mara kwa mara, Amani lina stori
kamili.
Mapema wiki hii, paparazi wetu alikuta gari
hilo likiwa limebuma mitaa ya Victoria,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku mshindi
huyo wa Shindano la Miss Tanzania mwaka
2006 akiwa ndani, lakini ili kukwepa aibu,
aligoma kutoka nje kuomba msaada, badala
yake akabakia ndani huku akijaribu kuwasiliana
na watu wake wa karibu.
Mmoja wa wasaidizi wake wa karibu, Petit Man
baadaye akitumia gari jingine alifika eneo hilo
akiwa ameambatana na fundi, ambao
walilisukuma hadi eneo salama na kuliegesha.
Wema alibakia ndani ya gari hilo wakati fundi
akijaribu kurekebisha dosari ambayo haikuweza
kufahamika mara moja.
Hadi gazeti hili linaondoka eneo hilo baada ya
juhudi za kumpata ili azungumze kugonga
mwamba, hakukuwa na dalili za kupatikana
kwa ufumbuzi.Mtu wa karibu na Madam
aliliambia gazeti hili kuwa gari hilo limekuwa
likimsumbua kwa muda mrefu kiasi kwamba
wakati mwingine hulikumbuka gari aina ya
Nissan Murano, ambalo alipewa na Diamond
siku hiyohiyo ya bethidei yake, lakini akaliuza
baada ya wawili hao kutofautiana.
Baadaye Wema alitafutwa kupitia simu yake ya
mkononi, lakini haikuweza kupatikana ili
azungumzie juu ya gari hilo, ingawa siku za
nyuma wakati gari hilo lilipokutwa likiwa
limetolewa matairi eneo la Komakoma,
alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa
anahisi BMW hilo lilikuwa limetumika sana
kabla ya kupewa kwa vile limekuwa
likimsumbua mara kwa mara.
GPL