Friday, July 17, 2015

Baada ya Lowassa KUKATWA........Vijana 30 wa CCM-Vyuo Kikuu Wahama na Kujiunga na CHADEMA


Vijana hao wakiwa katika Tawi la Chadema, Mwananyamala jijini Dar.
VIJANA takribani 30 wa vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), jana  wamesalimisha kadi zao za CCM katika tawi la Chadema lililopo Mwananyamala, jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa hawakuridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea wa urais wa CCM.
Mmoja wa vijana hao akichukua kadi yake ya Chadema.
*****


Vijana hao wa vyuo vikuu mbalimbali waliokuwa wakiimba wimbo wa tunaimani na Lowassa wamekabidhi kadi zao za CCM kwa Kaimu Mwenyekiti wa Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni ya Chadema, Bi. Esther Semaja na kukabidhiwa kadi za uanachama wa Chadema.