Monday, July 6, 2015

WEMA: NILITOA MIMBA MWAKA 2008, NAHOFIA SITAZAA TENA


“Ninatamani sana kuwa na mtoto na naona siku zinakimbia, naanza kuwa na wasiwasi kuwa pengine wakati mimba ile inatolewa labda kuna vitu vilikwenda kombo,” alisema Wema katika maongezi yake na kipindi cha Take One cha Clouds TV. 

Miss Tanzania wa mwaka 2008 na mkali wa filamu bongo, mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema aliwahi kutoa mimba mwaka 2008 na hiyo inaanza kumtia mashaka kuwa pengine anaweza asipate mtoto.

Wema amesema alikuwa bado mdogo na ndo kwanza alikuwa anaingia kwenye ujana, akashika mimba na akaamua kuitoa kwa kumhofia mama yake. Wema amesema bado hajakata tamaa ya kuwa na mtoto lakini ameanza kuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa ndoto yake hiyo kutimia.