Jengo la Maduka ya Westgate.
Jengo la maduka la westagate lililo katika Mji Mkuu wa Kenya Nairobi linafungua upya milango yake hii leo kwa umma baada ya kufungwa kwa kutumika miaka miwili tangu liliposhambuliwa na wanamgambo wa Al Shaabab Septemba 2013.
Watu 67 waliuawa wakati wa makabiliano ya siku nne wakati wanamgambo hao walipovamia maduka hayo na kuwafyatulia risasi watu waliokuwemo ndani ya maduka hayo, kwaua na wengine kujeruhiwa vibaya.
Namna ambavyo mashambulizi hayo yalivyotekelezwa na Al Shabaab.
Jengo hilo linafunguliwa wiki moja baada ya rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara nchini Kenya hatua inayoonekana kama ishara ya amani na usalama nchini humo.
Al Shabab wameendesha mashambulizi mengine mabaya nchini Kenya tangu litokee shambulizi la Westgate likiwemo la chuo kikuu cha Garissa ambapo watu wapatao 150 waliuawa.