Saturday, August 29, 2015

Wolper acharuka kisa mimba

jackline-wolper1
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper.
Imelda mtema
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper amecharuka vibaya mara baada ya kuulizwa habari za ujauzito.
Juzikati mwanahabari wetu alipenyezewa ubuyu kuwa mwigizaji huyo haonekani viwanja kwa kuwa ni mjamzito ndipo mwanahabari wetu alipomvutia waya Wolper ambaye alijibu kwa hasira.
“Nani kawaambia nina ujauzito? Hayo mambo jamani siyapendi. Sitaki kuyasikia. Kama nina ujauzito si ningesema? Nifiche ili iweje?” alisema Wolper.