Tuesday, September 29, 2015

VIOJA SOKA LA BONGO Siri zaibuka kiatu cha Msenegali Simba KUMBE KILIKUWA NA NANII..SOMA MWENYEW HAPA


STRAIKA Msenegali wa Simba, Pape N’daw amelitumia Mwanaspoti kusafisha kashfa iliyoenea mtaani kwamba anachezea viatu vya ndondo. Mchezaji huyo aliiambia Mwanaspoti jana Jumatatu kwamba; “Mimi nina viatu Pea tano.

“Pea nne ni mpya , mbili nilinunua Zanzibar na mbili nikanunua Dar es Salaam vipya kabisa. Kile nilichochezea kwenye mechi dhidi ya Yanga ndio huwa natumia kuchezea kwenye mechi zote, ndio kiatu changu cha mechi.

“Hizo Pea zingine nne ni kwaajili ya mazoezi na mambo mengine, kwahiyo wanavyosema natumia viatu chakavu nawashangaa.” Mchezaji huyo alisisitiza kwamba kiatu hicho anakipenda na anapenda kukitumia sikunyingi na atazidi kukitumia huku akionyesha viatu vingine vipya alivyovitumia kwenye mazoezi ya jana jioni katika uwanja wa Boko Veteren, Tegeta.

Lakini kocha wa Simba, Dylan Kerr, amewatazama nyota wake watatu; Jonas Mkude, Abdi Banda na Msenegali, Pape N’daw na kugundua kuwa nafasi zao zipo wazi katika kikosi chake lakini bado hawako fiti vilivyo kwa mapambano.

Katika kuhakikisha kuwa nyota hao wanakuwa fiti, Kerr amepanga kuwatafutia mechi nje ya zile za Ligi Kuu Bara ambapo jana Jumatatu timu yake hiyo ilicheza dhidi ya timu ya vijana ya Simba U-20 ili nyota hao waweze kuwa fiti.