Kwa upande wake mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuliimarisha jeshi la Tanzania ingawa zipo changamoto ndogo ndogo lakini anaamini serikali itazifanyia kazi ili kuweza kuwa na jeshi imara...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua uwanja wa ndege katika kambi ya kijeshi ya anga iliyoko Ngerengere mkoani Morogoro ambapo amesema anajivunia kutoka madarakani akiwa ameiacha nchi katika hali nzuri ya kiusalama.
Rais Kikwete akizungumza katika uzinduzi huo amesema katika kipindi cha uongozi wake amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuliacha jeshi likiwa katika hali nzuri ambapo ameeleza hakuna nchi inayoweza kuwa na maendeleo kama haina jeshi imara.