Friday, November 27, 2015

Kwa mashabiki wa Liverpool hizi sio habari njema kwa staa wao Daniel Sturridge …

Hizi haziwezi kuwa taarifa njema kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingerezaanayeichezea klabu ya Liverpool Daniel Sturridge ambaye hakupata nafasi ya kucheza wala kukaa benchi katika mchezo wa michuano ya UEFA Europa League usiku wa November 26 dhidi ya Bordeaux  katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield.
Staa huyo wa Liverpool ambaye alikuwa nje ya uwanja toka October 4 baada ya kuwa majeruhi na kulazimika kuwa nje ya kwa muda, alikuwa akitazamiwa kucheza mchezo waEuropa League usiku wa November 26 ila stori mpya ni kuwa nyota huyo ameshindwa kurejea uwanjani baada ya kuonekana bado alikuwa na tatizo.
Daniel Sturridge Liverpool Ramon Motta Besiktas
Daniel Sturridge mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikuwa akilalamika kuhisi maumivu katika mguu wake, amepata nafasi ya kucheza mechi tatu pekee msimu huu na 18 kwa mwaka 2015, alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Aston VillaSeptember 26 lakini bado hajapata nafasi ya kucheza chini ya kocha mpya Jurgen Klopp.