Wednesday, December 30, 2015

Majibu ya msemaji wa Simba Haji Manara kuhusu Simba kuhusishwa kumsajili Haruna Niyonzima (+Audio)

Siku moja baada ya klabu ya Dar Es Salaam Young African kutangaza maamuzi ya kuvunja mkataba na kiungo wake wa kimataifa wa Rwanda aliyekuwa anakipiga katika klabu hiyo Haruna Niyonzima. Mengi yameanza kuandikwa na kuulizwa eti klabu yaSimba inamnyatia staa huyo wa Rwanda? Hili ndio jibu la afisa habari wa Simba Haji Manara.
niyonzima-1
“Haruna Niyonzima ukiniuliza mimi hata viongozi wa Simba wanajua kuwa mimi nampenda sana Haruna Niyonzima ila ni mimi Haji Manara, ndio aina ya viungo ninaopenda wawe vile, lazima niseme nampenda lakini mimi sisajilii kazi yangu ni kupewa habari na kuja kuwaambia lakini sijapewa habari za Niyonzima”>>> Manara