Mbunge wa jimbo Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kortini Kisutu, jijini Dar es Salaam leo na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea.