Wednesday, January 20, 2016
A - Z YA TIMBWILI LA SHILOLE KIUNO NA NUH MZIWANDA STUDIO
Kimenuka mbaya! Gumzo kubwa mjini ni timbwili ‘hevi’ aliloliangusha Mbongo-Fleva wa kike, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au Shishi’ ndani ya Studio za Clouds TV mara tu baada ya kumuona aliyekuwa mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ katika zoezi la kutaka kuwapatanisha baada ya kutemana hivi karibuni hivyo mahojiano yakavurugika na kwamba upatanisho haukufanikiwa.
Mara tu baada ya kuchomoka kwenye ‘intavyu’ hiyo, Shilole alitimkia nchini Afrika Kusini (Sauz) lakini alipata nafasi ya kuzungumza na gazeti hili kuelezea kile kilichotokea.
Shilole alisema, hakuna siku amewahi kufikia wakati mgumu kama siku hiyo ambapo aliitwa na mmoja wa watangazaji wa Clouds TV, akimuomba wafanye mahojiano na akakubali akijua yatakuwa ni mahojiano ya kawaida yahusuyo muziki na shughuli zake zingine kama msanii wa kawaida.
Alisema kuwa kwa upande wake intavyu hiyo ilikuwa ngumu mno kwani hakutarajia na maswali yaliyomhusu Nuh Mziwanda ndiyo maana yakatokea yaliyotokea.
“Ile kugonga vitu na kutaka kutoka ilikuwa ni hasira kwani nilikwazika sana, ningejua mapema kuwa wameniita kukutanishwa na huyo Nuh kweli nisingeenda,” alisema Shishi.