Wednesday, January 20, 2016

Baada ya Shiole na Nuh Mziwanda Kukutanishwa, Je Kuna Uwezekano Wakarudiana?


Ijumaa iliyopita kupitia kipindi cha WikiendChartShow cha Clouds Tv kiliwakutanisha Nuh Mziwanda na Shishi ambao wameachana,Je? Kuna uwezekano wapenzi hao wakarudiana?

’Nimeficha mambo yake mengi sana kwa maslahi ya penzi letu,yeye anajua mambo gani aliyokuwa akinifanyia ambayo alikuwa hastahili kunifanyia kama mpenzi wake,alikuwa akinichukulia poa tu,nilikuwa nikionekana mwanaume mbele za watu lakini haikuwa kweli,nilikuwa naumia ndani kwa ndani bila watu kujua,nimemsamehe sina tatizo nae,’’Nuh.

‘’Nuh na Shishi ni marafiki zangu nawajua vizuri walipokuwa wakigombana nilikuwa niwasuruhisha yanaisha sasa kipindi hiki walivyogombana sikuwepo nilikuwa Kigoma,ningekuwepo yasingefikia haya ila ninachojua hawa wanapenda cha msingi mmoja wao ajishushe,’’Baba Levo.

‘’Unajua ukiongea na Nuh ukimuuliza unampenda Shilole hana jibu kamili lakini ninavyoona wanapenda na watarudiana tu,ila Nuh anawahofia ndugu zake ambao hawamtaki Shishi na mambo mabaya ambayo aliyokuwa akimfanyia,’’ Soudy Brown.