Kumbuka hili ni jumba lake binafsi na sio Ikulu ya Zimbabwe.
‘Blue House’ yenye vyumba vya kulala 25 ilijengwa na wahandisi wa kampuni ya ujenzi ya Serbia inayojulikana kama Energoproject na imetumia mchoro kutoka nchini China.
Mbali na hilo, unapaswa kufahamu kuwa jumba hilo limechukua eneo la hekari 44 na linalindwa kwa radar ya kisasa yenye thamani kubwa. Ndani lina ‘mabwawa mawili makubwa ya kuogelea’ ambayo wanayaoita ‘Maziwa’.
Endelea kuangalia picha: