Lucy Komba
Msanii wa kitambo kunako filamu za Kibongo, Lucy Komba anayeishi Finland kwa sasa, amezichapa ‘live’ na rafiki yake kipenzi, Edina John huku kisa kikitajwa ni wivu wa mapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mashosti hao, kilimwaga ubuyu kuwa mapema mwezi huu, Lucy alimualika rafiki yake huyo nyumbani kwake kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu mambo ya filamu, nk.
“Baada ya Edina kwenda kule walikuwa wakikaa nyumba moja na ikatokea mazoea makubwa kati ya mume wa Lucy na Edina kitu ambacho kilimpa wasiwasi Lucy.
“Siku ya tukio Lucy alikuwa jikoni akipika huku Edina akipiga stori na mumewe sebuleni, alipopiga chabo alimuona shosti wake akiongea kwa kumrembulia macho mumewe tena wakiwa karibu akamfuata na kumrushia maneno machafu na kushikana ndipo mumewe akawaamulia,” kilisema chanzo.
Baada ya Showbiz Xtra kunyaka ubuyu huo, lilimtafuta Lucy kwa njia ya WhatsApp ambapo alifunguka kwa kifupi;
“ Jamani hayo mambo yameshapita kwanza hayana hata maana kwenye gazeti kabisa.”
Edina alisema; “Nashangaa ni kitu gani kilimpata Lucy mpaka kufikiria mimi naweza kuwa na uhusiano na mume wake kitu ambacho hakitatokea nafikiri alishindwa kujiamini tu.”