Wednesday, March 23, 2016

Mastaa na ‘ugonjwa’ wa tuzo kitandani

11199470_1002922379731138_968098397_n
Chibu akiwa amelala na tuzo.
DUNIANI kote, mastaa ndiyo watu wenye kuanzisha jambo ambalo baadaye husambaa kwa mashabiki na hata watu wa kawaida mitaani.Utakumbuka staili ya uvaaji wa suruali chini ya makalio, maarufu kama Kata K, ilianzia kwa wanamuziki maarufu nchini Marekani.
Baadaye mtindo huo ukasambaa haraka kiasi kwamba hadi hivi sasa, unapopita Manzese ‘ndanindani’ huko, unakutana na watu ambao hawajawahi hata kufika Dar Live kuangalia shoo, lakini wakiwa wamepiga Kata K! Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wasanii wa Bongo,
baada ya hivi sasa kuzuka kwa mtindo wa watu wanaoshinda tuzo, kupiga picha wakiwa wamelala nazo kitandani, hii ikiwa ni mara tu baada ya kinara wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ kuanzisha kufuatia ushindi wa tuzo yake ya MTV MAMA 2015, PALE Durban, Afrika Kusini.
lulu3422Lulu na tuzo yake.
Wafuatao ni mastaa na maelezo ya tuzo walizoshinda, ambao picha zao zinawaonesha wakiwa wamelala nazo vitandani.
DIAMOND
Huyu ndiye staa aliyefungua milango ya wasanii kufanya hivyo kwani baada ya kupata Tuzo ya MTV MAMA 2015 katika kipengele cha Mtumbuizaji Bora zilizofanyika jijini Durban nchini Afrika Kusini, siku chache baadaye picha iliyomuonesha akiwa amelala kitandani na tuzo hiyo ilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
mbwanaMBWANA SAMATTA
Mwanasoka bora zaidi kwa sasa nchini, Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji, alipiga picha iliyomuonesha amelala kitandani, akijifunika bendera ya taifa, mara baada ya kushinda
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani 2015, zilizotolewa jijini Abuja, Nigeria Januari mwaka huu.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ Huyu alishinda Tuzo za African Movies Viewers Choice (AMVC) zilizofanyika nchini Nigeria katika Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Mapenzi ya Mungu) ambapo alipiga picha akiwa amelala nayo kitandani pembeni yake kama walivyofanya wenzake.
12356522_904899752926768_2056221279_nDAX HANNZ Huyu ni kijana Mtanzania anayeishi nchini Afrika Kusini anakojishughulisha na uanamitindo (Modeling) ambapo mwaka jana alipata Tuzo ya Mwanamitindo Bora wa Mwaka 2015 (Model of the Year) ambazo zilitolewa na Abryanz Style and Fashion Award (ASAF 2015) zilizofanyika nchini Uganda ambako Diamond na Zari pia walipata tuzo ya ‘Most Stylish Couple’.