Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
MKURUGENZI wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, leo kupitia kipindi cha Power Breakfast amekanusha uvumi wa watangazaji wa kituo hicho, Gerald Hando, Abel Onesmo na PJ, kuacha kazi.
“Kwa nafasi yangu kama mkurugenzi, taarifa nilizonazo ni kwamba tuna mikataba na wafanyakazi hao ambayo inaisha leo tarehe 31. Sehemu kubwa ya wafanyakazi wetu mikataba yao inaisha mwezi huu, hivyo katika hali ya kawaida huwa tunatoa nafasi ya kumwambia anayetaka kuendelea na mkataba aandike barua au aseme,” alisisitiza Mutahaba.