Saturday, April 2, 2016

Diamond Aingia Studio Na Fally Ipupa, Achill Na Awilo Longomba


Likizo ya Diamond Platinumz na familia yake jijini Paris Ufaransa sio likizo ya kulala na kula bata tu bali ya kuisaka dunia mpya na kufanya kazi kubwa zaidi.
Mwimbaji huyo ametumia nafasi hiyo kukutana na nguli wa muziki wa lingala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Fally Ipupa na kuingia naye studio kupika kazi mpya.
“Music doesn’t sleep… with my Brother @diamondplatinumz,” Fally Pupa ameandika Instagram kwenye picha inayomuonesha akiwa na mwimbaji huyo mzawa wa Tandale jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, kwa mara ya kwanza Diamond amekutana na Mkongwe wa Lingala, Awilo Longomba na wawili hao wamezungumza ‘kitu’, huku Zari the Boss Lady akishawishi kufanyika kwa biashara ya muziki kati yao.
“My good friend @awilolongomba came to visit, hope you do some business with hubby. Was great,” ameandika Zari.
Awilo Longomba na Diamond, Zari
Kumbuka hivi karibuni Awilo alifanya kazi na ‘P-Square’ hivyo ukawa muziki wa Lingala umekutana na muziki wa kizazi kipya.
Msanii mwingine wa kizazi kipya aliyepata shavu la Awilo Longomba, ni Mnaija Chidinma.