Tuesday, May 31, 2016

Ukweli Wa Taarifa Za Kipre Tchetche Kusaini Oman, Umeelezwa Na C.E.O Wa Azam FC



Baada ya kuenea kwa habari za mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Azam FC Kipre Tchetche kuripotiwa kusaini klabu ya Nahda Al-Buraimi ya Oman, afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ameeleza ukweli na kuwatoa hofu mashabiki walioshtushwa na habari hizo.
C.E.O wa Azam FC Saad Kawemba kaeleza kuwa hizo ni habari za uzushi za kuwa nyota wao amesaini Nahda Al-Buraimi ya Oman, kwani bado ana mkataba na Azam FC ndio maana hata vyombo vya habari vinaripoti kuwa anaomba akapate changamoto mpya kwa maana ana mkataba na Azam FC.
12998153_1164821906891497_8966146697048225476_o-800x546
“Kipre ni mchezaji wetu ambae ni muhimu huwezi kumruhusu amalize msimu aende mapumziko akiwa hana mkataba, kwa hiyo tuna mkataba ambao ni endelevu, nadhani ndio maana ukasikia wanasema anaomba akapate changamoto sehemu nyingine, ukweli ni kuwa mchezaji kama ana mkataba ni makubaliano umuuze au anunue mkataba”