siku chache zilizopita iliripotiwa kuhusu kikundi cha wanamgambo cha somalia cha al-shabaab kuzuia matumizi ya internet pamoja na simu za gharama aina ya smartphone.. kwa mujibu wa wasemai wa kikundi hicho kilichotekereza mauaji ya westgate kinadai kuwa watu utumia smartphone kuvujisha siri kwa maadui wa kikundi hicho kinacho miliki baadhi ya maeneo nchini humo.. baadhi ya watu wameshuhudia jinsi vijana wa al-shabaab walivyopitisha msako majumbani mwao.. takribani vijana kama wanne walikuja kwenye famasi yangu na kukuta simu yangu aina ya samsung galaxy ikiwa inachajiwa ndipo waliniamru kuwapa simu hiyo , hapo hapo walianza kupekua inbox na sent item ya simu yangu huku wakiniuliza maswali yasiyokuwa na msingi kama nliaapataje hiyo simu.. na kama nimetuma ujumbe nje ya nchi,, niliwajibu majibu wanayoyataka nikasema huwa siwasiliani nje ya somalia... alisema Hassan Farah ambaye ni mkazi wa mji wa Barawe
Farah alisema vijana hao walimwambia hasitumie smartphone tena kwani zinatumika kuwakandamiza waislam
nae mama mmoja ambaye alitaka aitwe jina moja tu la sarah alisema kuwa .. kuzuiwa kwa smartphone sio kitendo cha kiungwana kwani kinapingana mna maendeleo ya sayansi na teknolojia... akaongeza pia kuwa ni kusababisha usumbufu kwa wananchi na kuzorotesha uchumi wa nchi.